Tuesday, 18 August 2020

NOVENA KWA MT. MONIKA

NOVENA KWA MTAKATIFU MONIKA MZAZI WA MT.AGOSTINO


Kwa jina la Baba...

TUOMBE.

Mt. Monika, mwanamke na mama mwenye kuteseka, unajua machozi yangu, mahangaiko na uchungu wangu. Wakati fulani uliteseka kama mimi; naomba unionee huruma kwa mateso niliyonayo, Uniombee. Kutoka kwa Roho Mtakatifu ulipokea zawadi ya ufahamu na busara nguvu na sala. Uniombee ili nami nijaliwe zawadi zilezile. Kwa kuwa ulikuwa mpatanishi, daima uwaombee mume na watoto wangu na usali kwa ajili ya amani ya nyumba yetu.

Kwa maombezi yako uliwaokoa mumeo na mwanao. Utuombee neema ya Mungu ili tuwe na imani katika nyumba yetu. Kutokana na kuhudhuria Misa kila siku uliweza kupata nguvu na faraja; basi utuombee nasi nguvu na faraja katika maisha yetu daima. Utuombee kwa ajili ya mahitaji yetu muhimu ya kidunia; kusudi tuweze kufanya kazi na kuwa na amani katika familia yetu. Uwakumbuke watoto wangu, ili daima wajue pendo la kweli na hivyo wamtumikie Mungu kwa mapendo safi. Uniombee, ili niwe mama mwema kwao, na mwisho wa maisha haya, mimi pamoja na mume wangu, watoto wangu na wapendwa wangu wote tuweze kufika kwa Mungu, huko ambako wewe upo pamoja na mume wako na watoto wako wote. Kwa njia ya Kristo, Bwana wetu. Amina.

*Sala kwa mtakatifu monika*

Kumbuka,  mpendwa mtakatifu MONIKA furaha iliyo furika moyoni mwako Augostino :Mwanao kwa maombi yako na machozi alipogeuza maisha yake na kumpokea Bwana. Tafadhali tupelekee maombi yetu mbele yake mungu ambaye kwake mwanao amesimama. Pokea kwa niaba yetu iwapo yatakuwa mapenzi  yake Mungu neema tunaomba kwa unyenyekevu kupitia kwa nguvu za utetezi wako ili tuweze kuona na kufurahia matokeo ya maombi yetu 
Tunaomba hayo kwa njia ya kristu Bwana wetu anayeishi na kutawala milele na milele

*SALA KUJIKABIDHI KWA MT.MONIKA*

Ee Mpendwa Mtakatifu Monika, tunakuomba sana utuangalie kwa macho ya huruma sisi tunaoomba msaada wako. Tunaomba upokee nia zetu hizi tunazokuletea ( *taja nia yako hapa* ) uzipokee na ututimizie. Tunaimani kubwa kwako na Katika uwezo wako wa maombezi. Katika safari hii ya siku tisa tunakuomba kwa unyenyekevu upokee na kuzichukua sala zetu na kuzikabidhi kwa Mungu Amina. 

Tunakimbilia ulinzi wako…
Salamu Maria...
Baba Yetu...
Atukuzwe Baba...
Kwa jina la Baba...

*Mt. Monika, Mlinzi wa akina mama Wakristo. Utuombee.*

( IMENAKILIWA NA SHEMASI SAMUEL NYONJE) 

samnyonje.blogspot.com