Tuesday, 2 June 2020

NOVENA KWA MTAKATIFU ANTONIO WA PADUA

NOVENA KWA MTAKATIFU ANTONIO WA PADUA

PAROKIA YA MTAKATIFU ANTONIO WA PADUA DCK: JIMBO KATOLIKI NAKURU

3rd 12th June 2020

JUMATANO: 3rd June: Historia ya Mtakatifu Antonio wa Padua

Mt Anthony wa Padua alizaliwa mwaka 15th Agust 1195 huko Lisbon,Ureno.Aliitwa

Fernando Martins.Alizaliwa katika familia njema yenye uwezo.Akiwa na umri wa miaka

15,aliomba kupelekwa seminari ya Santa Cruz katika mji wa Coimbra,ambako alisoma

teolojia na kilatini.

page1image3392

Akapata daraja la upadre,na akawa hapo hapo mjini Coimbra.Wakaja Wa franciscan ambao

page1image3920

walitengeneza makao yao nje ya mji.Padre Fernando Martin akawapenda,akaomba ruhusa ili

page1image4428

ajiunge nao.Aliporuhusiwa akajiunga nao,akabadili jina,akaitwa Anthony.

Akasafiri mpaka Morocco,kueneza neno la Mungu.Huko akaugua sana,ikabidi arudishwe

Coimbra kwa matibabu.Chombo alichopanda kilivunjika kwa dhoruba,hata hivyo Mtakatifu

Antonio alifika Sicily, na akapelekwa katika mji wa Tuscany ili apate matibabu na

mapumziko.Wakati akiendelea na matibabu,alitumia muda wake mwingi akisali na kusoma.

Muda huo pia walipata wageni ambao walikuwa Wa Dominican. Kukawa na hali ya

kutegemea kila upande kutoa mahubiri. Mkuu wa Wa franciscan alimwambia Mtakatifu

Antonio atoe mahubiri kadiri Roho Mtakatifu atakavyomjaalia. Akatoa mahubiri

yaliyowagusa wote,na kuwasisimua mno.

Habari za mahubiri hayo zikamfikia Mtakatifu Francis wa Assisi,ambaye alipomuona

Mtakatifu Anthony wakawa marafiki. Mt Anthony alikuwa na kitabu cha zaburi,ambacho

ndani yake kulikuwa na mafundisho ya ufafanuzi kwa wanafunzi. Kitabu hicho kwake

kilikuwa kitu chenye thamani mno.Mwanafunzi mmoja aliamua kutoroka seminarini,akaiba

na kitabu hicho.Mt Anthony alisali akiomba kitabu hicho kipatikane na kirudi kwake.Lakini

yule aliyekiiba alirudi nacho,akamrudishia.Kitabu hicho kimehifadhiwa katika kanisa la

Bologna hata sasa.

Mt Anthony aliendelea, kuhubiri na kufundisha katika miji mbalimbali; Ufaransa na Italia.

Kuna wakati aliamua kwenda mtoni, akahubiria samaki baada ya watu kukosa kusikiliza

mahubiri yake.Watu walivyogundua utulivu na usikivu wa samaki nao wakakusanyika na

kusikiliza.

Mt Anthony alifariki mwaka wa 13th June 1231.Akatangazwa Mtakatifu Siku 336 baada ya

page1image14732 page1image14816

kifo chake na Papa Gregory wa IX. Mwaka 1946 Papa Pio wa XII alimtangaza Mtakatifu

page1image15404

Antonio kuwa Daktari wa kanisa.

1

SIKU YA KWANZA : Alhamisi 4th June Kituo: St. John Maiella + St. Ann- Ngondi

Kwa jina la Baba na la Mwana, na la Roho Mtakatifu...

Ee Mtakatifu Antonio wa Padua, mnyenyekevu kwa watakatifu, upendo wako kwa Mungu na ukarimu duniani ilikustahilisha hapa duniani kupewa nguvu za miujiza. Miujiza mingi ilifanyika kwa nguvu za Kristu kupitia kwako, na wengi walisubiri kwa neno hilo ambalo ulikuwa tayari kusema.

Tukitumainia haya, twaomba utujalie neema tuombao kwa Mungu kupitia novena hii ( taja nia ). Majibu ya sala zetu twaamini zitafanyika kwa miujiza maana wewe pia ni mtakatifu wa miujiza. Ee Mnyenyekevu na mpendevu mtakatifu Antonio wa Padua, roho yako ilijawa na huruma kwa ulimwengu, tunakuomba ukaribishe sala zetu kwa Mtoto Yesu aliyependa kukaa mikononi mwako, na mwisho furaha ya mioyo yetu iwe kwako, kwa Kristu Bwana wetu...Amina

Baba yetu...........Salamu Maria.......Atukuzwe Baba..... Mtakatifu Antonio......Utuombee

SIKU YA PILI: Ijumaa 5th June
Kituo: Mtakatifu Patrick + Our Lady Moindabi
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu...Amina

Ee mtenda miujiza Mtakatifu Antonio wa Padua, kumbuka kwamba, hakuna aliyeachwa bila usaidizi kwa maombezi yako. Tukijazwa na nguvu hii, tuna ujasiri kukimbilia ulinzi na maombezi yako ee rafiki wa Yesu, ee mhubiri wa huruma ya Mungu, usitazame unyonge wetu bali yafikishe maombi yetu katika kiti cha enzi cha Mungu, yatie nguvu kwa maombezi yako na utujalie neema tuombayo katika novena hii ( taja nia hapa ). Amina

Baba yetu....Salamu Maria....Atukuzwe Baba... Mtakatifu Antonio wa Padua...Utuombee

page2image6876 page2image6960 page2image7044 page2image7128 page2image7212 page2image7296

2

SIKU YA TATU: Jumamosi 6th June

Kituo: Mtakatifu Thomas + Mtakatifu Elizabeti

Ee Mtakatifu Antonio wa Padua, msafi, ambaye katika uadilifu wako ulijaliwa kwa neema ya Mtoto Yesu, kumshika katika mikono na rohoni mwako. Tunakuomba utujalie hili tukuombalo.

Ee mtukufu Antonio wa Padua, ulizaliwa chini ya ulinzi wa Maria Mtakatifu, na katika kupalizwa kwake mbinguni amekuwa kwetu mwombezi na kimbilio letu, tunakuomba utuombee neema tuiombayo katika novena hii ( taja nia hapa ). Tuombee ee Mtakatifu Antonio mfanyikazi mkuu na mtenda miujiza ili Mungu ayajibu maombi yetu. Amina

Baba yetu........Salamu Maria.....Atukuzwe...... Mtakatifu Antonio wa Padua.... Utuombee

SIKU YA NNE: Jumapili 7th June
Kituo: Mary Immaculate + Teresa Ndabibi

Baba yetu...Salamu Maria...Atukuzwe Baba... Mtakatifu Antonio wa Padua....Utuombee

SIKU YA TANO: Jumatatu 8th June
Kituo: Mary Immaculate + St. Mark
Kwa jina la Baba ,na la Mwana, na la Roho Mtakatifu...

Tunakusalimu na kukuheshimu, Ee msaidizi mwenye nguvu, Mt.Antonio wa Padua.

Ulimwengu wa Kikristo unakuelekea na kupata uzoefu wa huruma yako na msaada wa nguvu

katika mahitaji mengi, na mateso ambayo tumehamasisha katika haja yetu ya kutafuta

msaada wako. Twakuomba ili tupate jibu nzuri kwa ombi letu la neema tunalotafuta katika

novena hii (taja nia yako hapa). Ee Mtakatifu Antonio wa Padua, nakusihi, nipate neema

ambayo natamani kwa maombezi yako. Amina.

Tunakusalimu ee Mtakatifu Antonio wa Padua, msafi naPambo la utukufu wa Ukristo.

Tunakusalimu, Mtakatifu mkuu, kerubi wa hekima na upendo wa Mungu. Hakika twafurahi

kwa neema aliyokupa Mungu wetu. Kwa unyenyekevu na ujasiri Ninakuomba unisaidie,

kwani ninajua kwamba Mungu amekupa upendo na huruma, pamoja na nguvu. Ninakuuliza

kwa upendo ambao wewe huhisi kwa Yesu mtoto mchanga ilivyofanyika katika mikono

yako, mweleze sasa atupe neema tunayotafuta kupitia maombi yako katika novena hii (taja

nia yako hapa).

3

Baba yetu...Salamu Maria...Atukuzwe Baba... Mtakatifu Antonio wa Padua... Utuombee

SIKU YA SITA: Jumanne 9th June
Kituo: St. Catherine + St. Raphael
Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu...

Ewe mtukufu Mtakatifu Antonio wa Padua, ulichaguliwa na Mungu kuhubiri neno lake.

Ulipokea kipaji cha kunena kwa ndimi na nguvu ya kufanya kazi ya miujiza kutoka kwa

Mungu. Ewe Mtakatifu Antonia mwenye heri, niombee nitimize wajibu wa Mungu kwa yote

ili nimpende nawe katika milele yote.

page4image3984

Ee Mtakatifu Antonio wa Padua mkarimu, nakuomba uniombee neema ninayotamani kupitia

page4image4492

novena hii ( taja nia yako hapa). Amina

Baba yetu...Salamu Maria...Atukuzwe Mungu... Mtakatifu Antonio wa Padua...Utuombee

SIKU YA SABA: Jumatano 10th June
Kituo:St. Kizito + St. Elizabeth
Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu...

Baba yetu...Salamu Maria...Atukuzwe Baba... Mtakatifu Antonio wa Padua...Utuombee

page4image6748

Ee Mtakatifu Antonio wa Padua uliye maarufu na bingwa katika imani na miujiza mingi

page4image7316

iliyotendeka kwako. Naomba uniombee katiku ukuu wa Bwana Yesu neema ninazohitaji

page4image7824

kupitia novena hii ( taja nia yako hapa).

page4image8272

Ee Mtakatifu Antonio wa Padua, uliye makini kwa wote wakuombao, nipe msaada kwa

page4image8820

maombezi yako yenye nguvu. Amina.

4

SIKU YA NANE: Alhamisi 11th June
Kituo: St. Joseph & St. John Mirera
Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu...

Mtakatifu Antonio wa Padua, wewe umeonyesha mwenyewe nguvu katika maombezi yako,

hivyo zabuni na uonyeshe huruma kwa wale wanaokuheshimu na kuomba katika mateso na

dhiki. Nakuomba sana kwa unyenyekevu na kwa dhati kunichukua mimi chini ya ulinzi wako

katika mahitaji yangu ya sasa na kupata kwangu neema ninayoomba katika novena hii (taja

nia yako hapa).

page5image3984

Pendekeza ombi langu kwa malkia wa mbinguni mwenye rehema, ili aweze kusihi sababu

page5image4532

yangu pamoja nawe mbele ya kiti cha enzi cha Mwana wa Mungu. Amina

Baba yetu...Salamu Maria...Atukuzwe Baba... Mtakatifu Antonio wa Padua...Utuombee

SIKU YA TISA: Ijumaa 12th June Kituo: St. Anthony of Padua Dck

Mtakatifu Anthony, mtumishi wa Maria, utukufu wa Kanisa, tuombee kwa ajili ya Baba yetu Mtakatifu, Askofu wetu,Mapadre,Mashemasi, Waseminari,Watawa wa kike na wa kiume, na waalimu wa dini, ili kwamba, kwa njia ya juhudi zao za kumcha Mungu na kazi ya kitume,

wote wanaweza kuwa Umoja katika imani na kutoa utukufu zaidi kwa Bwana.

page5image8040

Mt. Antonio wa Padua Msaidizi wa wote wanaokuomba, niombee kwa Mungu mbele ya kiti

page5image8608

chake cha enzi ili nitunukiwe neema katika novena hii ( taja nia yako hapa). Amina.

page5image9196

Baba yetu...Salamu Maria...Atukuzwe Baba...

page5image9564

Mtakatifu Antonio wa Padua...Utuombee

SHEREHE NI JUMAMOSI 13th . MTAKATIFU ANTONIO WA PADUA

Na iruhusiwe kupigwa chapa: Rev.Fr. Jude

Ikatafsiriwa kwa Kiswahili na: Shemasi Samuel Nyonje katika: samnyonje.blogspot.com

page5image11000

Imenakiliwa kwa Kiingereza kwenye:

page5image11368

https://www.ewtn.com/catholicism/devotions/novena-to-st-anthony-of-padua-302

page5image11676

No comments:

Post a Comment