NOVENA KWA MTAKATIFU RITA wa CASCIA.
Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu...
Ee Mtakatifu Rita, mfanyakazi wa miujiza, kutoka patakatifu pako kule Kashia , ambapo katika uzuri wako wote unapumzika kwa amani, ambapo sanduku lako lipo na mapambo yako, nitazame kwa huruma mie ninakulilia na kuhuzunika. Tazama moyo wangu unavyovuja damu na kuzingirwa na miiba. Ee mpendwa Mtakatifu, kwamba macho yangu hayana machozi tena ya kumwaga, nimelia na kuhuzunika sana moyoni mwangu, nimefadhaika. Nahisi kwamba sala zangu zafa katika ulimi wangu. Nitakata tamaa katika mahangaiko haya?
Njoo kwangu, njoo ee Mtakatifu Rita unisaidie, wewe unayeitwa Matakatifu wa mambo magumu, mshauri wa waliokata tamaa,
Niombee kwa Mungu neema ninazoomba kupitia Novena hii
taja nia yako hapa
Kila mtu anasifu utukufu wako, kila mtu anaelezea miujiza ya ajabu sana inayotendeka kupitia maombezi yako, lazima mimi peke yangu niwe na tamaa kwa sababu hujanisikia? Ah hapana! Niombee basi kwa Bwana Yesu kwamba yeye akiongozwa na huruma na matatizo yangu na kwamba, kwa njia yako, Ee Mtakatifu. Rita, nipate kupata matamanio ya moyo wangu. Amina
Baba yetu...x 3
Salamu Maria ... x 3
Atukuzwe ... x 3
Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu...
No comments:
Post a Comment