LITANIA YA HURUMA YA MUNGU.
Bwana utuhurumie – Bwana utuhurumie.
Kristu utuhurumie – Kristu utuhurumie.
Bwana utuhurumie – Bwana utuhurumie.
Kristu utusikie – Kristu utusikilize.
Baba wa mbinguni Mungu – utuhurumie
Mwana Mkombozi wa dunia Mungu - utuhurumie
Roho Mtakatifu Mungu - utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu mmoja –utuhurumie.
Huruma ya Mungu iliyo sifa kuu ya Muumba wetu~Tunakutumainia (iwe kiitikio mpaka mwisho)
Huruma ya Mungu iliyo kilele cha ukamilifu wa Mwokoziwetu.
Huruma ya Mungu iliyo upendo usiopimika wa RohoMtakasa.
Huruma ya Mungu fumbo lisilofahamika la Utatu Mtakatifu
Huruma ya Mungu iliyo ishara ya uwezo mkuu wa MunguMwenyezi.
Huruma ya Mungu iliyofumbuliwa katika kuziumba Roho zaMalaika wa mbinguni.
Huruma ya Mungu iliyotuumba na kutuamuru tuwepo bilakutokana na chochote.
Huruma ya Mungu inayotujalia maisha ya kutokufa.
Huruma ya Mungu inayotukinga na adhabu tunazostahili.
Huruma ya Mungu inayotuinua tutoke katika taabu, unyongena maumivu ya dhambi zetu.
Huruma ya Mungu inayotufanya wenye haki katika Nenoaliyejifanya Mtu.
Huruma ya Mungu inayofurika kutoka katika majeraha yaKristu.
Huruma ya Mungu inayobubujika kutoka ndani ya MoyoMtakatifu wa Yesu.
Huruma ya Mungu iliyotupatia Bikira Maria Mtukufu awe kwetu Mama wa Huruma.
Huruma ya Mungu iliyoonyeshwa katika kuanzishwa KanisaKatoliki.
Huruma ya Mungu inayopatikana katika mafumbo yaSakramenti Takatifu.
Huruma ya Mungu inayotolewa kwa wanadamu wote kwanjia ya Sakramenti ya Ubatizo na Kitubio.
Huruma ya Mungu inayotolewa katika Sakramenti ya Ekaristina Upadrisho.
Huruma ya Mungu inayoonyeshwa kwetu pale inapotuita nakutuingiza katika kuwatakatifuza wenye haki.
Huruma ya Mungu inayotimilika katika ukamilifu wa watuwatakatifu.
Huruma ya Mungu chemchemi ya afya kwa wagonjwa nawote wanaoteseka.
Huruma ya Mungu iliyo faraja ya wote wenye uchungumoyoni.
Huruma ya Mungu iliyo tumaini la roho zinazosumbuliwa namkato wa tamaa.
Huruma ya Mungu iliyo mwenzi wa daima na popote wa watuwote.
Huruma ya Mungu inayowahi kutuletea neema zake.
Huruma ya Mungu iliyo amani yao wanaokufa.
Huruma ya Mungu iliyo burudisho na faraja yao marehemuwa toharani.
Huruma ya Mungu iliyo furaha ya mbinguni kwa watakatifuwote.
Huruma ya Mungu iliyo taji la watakatifu wote.
Huruma ya Mungu chemchemi ya miujiza isiyokauka.
Mwanakondoo wa Mungu uliyetuonyesha huruma yako kuukatika kuikomboa dunia kwa msalaba wako mtakatifu, ~ Utusamehe Ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu unayejitolea kwetu kwa mapendona huruma katika kila adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu, ~ Utusikilize Ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu anayeondoa dhambi za dunia kwanjia ya huruma yako isiyo na mwisho ~ Utuhurumie.
Kiongozi: Bwana utuhurumie –
Wote: Kristu utuhurumie, Bwana utuhurumie.
Kiongozi: Huruma anana za Bwana zi juu ya kazi zake zote –
Wote: Huruma za Bwana nitaziimba milele.
Tuombe:
Ee Mungu uliye na huruma isiyo na mwisho, na hazina zawema na upendo wako hazina mipaka. Tunakusihi ututazamesisi watu wako huku duniani na kutuongezea huruma yakotena na tena, ili itusaidie tusije tukakata tamaa hata maramoja, haidhuru tukumbane na majaribu makubwa kiasi gani, bali tuweze daima kuzielekea na kuzishika amri zako, kwamatumaini na kutimiza mapenzi yako matakatifu, ambayondiyo huruma yenyewe. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristu Mwanao, Mfalme wa Amani na Huruma, aishiye na kutawala nawe, na Roho Mtakatifu, kwa pamojamkituonyesha huruma, daima na milele. Amina.
Imetayarishwa na Shemasi Samuel Muhanji Nyonje. 0708607911 / nyonjes146@gmail.com
No comments:
Post a Comment