Sala ya Mtakatifu MIKAELI Dhidi ya Shetani na Hatari
Ee Mt. Mikaeli, Malaika Mkuu, utukinge miili yetu pamoja na roho zetu kutokana na maovu ya adui shetani, kundi lake lote na yeyote atakaye tusogelea na nia ya kutaka kutudhuru. Utukinge, na miili yetu, vyombo vya kusafiri, wakatitunaposafiri sehemu mbalimbali katika shughuli za kilasiku.Ukinge miili yetu, nyumba zetu, mali yetu, na vyombovyetu vyote hasa wakati wa kimbunga kikali, hatari za umemeza radi, upepo mkali, mvua kuu, na mafuriko ya maji. Zaidi yayote, tuko he dhidi ya ndoto chafu na muovu anayetakakuharibu nyoyo zetu. Wewe uliyemshinda Shetani, nipiganienami nimshinde yule muovu. Amina
NOVENA KWA MTAKATIFU MIKAELI MALAIKA MKUU
Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu...
Atukuzwe Baba na Mwana, na Roho Mtakatifu...
Ee Mtakatifu Mikaeli, Malaika Mkuu, Mshindi na mwaminifukwa Mungu na watu wa Mungu, Ninakuja mbele zako namatumaini makubwa nikiomba msaada wako wa haraka. Kwaajili ya upendo wa Mungu Baba ambaye amekujalia neema yanguvu zisizo na kifani, na kwa upendo wa Mama wa Yesu, Malkia wa Malaika wote, usiyakatae maombi yangu. Kwakuwa wajua jinsi moyo wangu ulivyo na thamani machoni pa Mungu Baba, nakuomba unilinde ili hata chembechembe zadhambi na uchafu za yule mwovu zisije zikaharibu umbo nzuri wa moyo wangu. Uniepushe daima na majaribu navishawishi vya shetani na mapepo wabaya. Ee Mt. Mikaeli, utiifu wako wa dhati kwa Mungu na Mama Kanisa takatifu, na upendo wako kwa Mungu na Kwetu ni wakutamanisha nawapaswa kuigwa. Kwa kuwa ndiwe mjumbe mkuu wa Munguunayetunza na kulinda watu wake, ninakuomba...
taja Ombi lako kwa Kimya kidogo
Ee Makatifu Mikaeli, kwa kuwa ndiwe muombezi na mtetezimkuu wa wakristu, Ninaamini kuwa kulingana na mapenzi yaMungu, Ombi langu litajibiwa.
Ninawaombea pia wapendwa wangu wote, utukinge kutokanana Hatari zote za mwili na Roho. Tusaidie na mahitaji yetu yakila siku, ili tuishi pia maisha matakatifu kupitia kwamaombezi yako ya ajabu, na mwisho tupate pumziko la furahambinguni, pamoja tumsifu na kumpenda Mungu wetu daimana milele Amina.
Kwa kutoa shukrani kwa Mungu kwa neema alizomjalia Mt. Mikaeli Sema:
Baba Yetu ...1
Salamu Maria ...1
Atukuzwe Baba...1
LITANIA YA MTAKATIFU MIKAELI MALAIKA MKUU
Bwana utuhurumie- Bwana Utuhurumie
Kristo Utuhurumie,
Bwana utuhurumie,
Kristo Utusikie,
Baba wa mbinguni Mungu, utuhurumie Mwana mkomboziwa dunia Mungu -
Roho mtakatifu Mungu Mmoja -
Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja -
Maria Mtakatifu - Utuombee
Malkia wa Malaika -Mtakatifu Mikaeli malaika Mkuu-
Msimamizi na mtetezi Mkuu wa imani na Dini takatifu-
Unaesimama upande wa kulia wa altari na ubani- Balozimkuu wa Paradiso- Mkuu wa majeshi ya Mbinguni-
Kiongozi wa Malaika wateule-
Ameri jeshi mkuu wa majeshi ya Mungu-
Mlinzi wa Neema takatifu, Mtetezi wa kwanza wa Ufalme waKristu-
Mwenye nguvu za kipekee za Mungu-
Jeshi mteule asiyeweza kuonekana kwa macho yakibinadamu-
Malaika wa Amani- Muongozo wa Kristu- Mlinzi wa ImaniKatoliki-Mshindi wa watu wa Mungu-
Malaika Mlinzi wa Ekaresti Takatifu-
Mtetezi wa Kanisa-
Mlinzi wa wadhifa wa Baba Mtakatifu-
Malaika wa amri za Kanisa katoliki-
Mwombezi wa wakristu- Mlinzi wa wote wanaomtumainiaMungu- Mlinzi wa Mwili na Nyoyo zetu-
Mponyaji wa wagonjwa- Mfariji wa wenye uchungu-
Mfariji wa Nyoyo zilizoko toharani-
Mhifadhi wa nyoyo zenye usafi-
Tisho dhidi ya mapepo wabaya-
Mshindi wa vita dhidi ya Shetani-
Mlinzi na Msimamizi wa Kanisa takatifu ulimwenguni-
Mwana Kondoo wa Mungu uondoae dhambi za Dunia- Utuopoe Ee Bwana Mwana Kondoo wa Mungu UondoaeDhambi za Dunia-Utusikilize Ee Bwana.
Mwana Kondoo wa Mungu Uondoae dhambi za Dunia, Utuhurumie.
K. Utuombee Ee Mtukufu, Mt Mikaeli Mkuu wa Kanisa la Yesu Kristu;
W. Ili tustahili ahadi za Kristu.
Tuombe
Ee Mungu Mwenyezi na wa Milele, Kwa wema na huruma yako ya ajabu umetaka watu wote waokoke, ukamweka Malaika Mikaeli kuwa Mkuu wa Kanisa Lako. Utukinge na adui zetu, wasitusumbue saa ya kufa kwetu, bali tuongozwe naye kwenye utukufu wako Mkuu. Tunaomba kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina
--
No comments:
Post a Comment